MSAFARA WA MR MOHAMED


Msafara wa Mh. Mohammed Dewji na Diamond Platnumz a.k.a Chibu Dangote ukiondoka katika viwanja vya People's Club.
Na Modewjiblog team, Singida
MBUNGE wa Singida Mjini na mfanyabiashara maarufu nchini, Mohammed Dewji amesema hatagombea ubunge wa jimbo hilo tena baada ya kulitumikia kwa miaka 10 na kuwezesha maendeleo makubwa katika sekta ya elimu na afya.
Mbunge huyo alisema hayo akihutubia maelfu ya wananchi waliokusanyika katika uwanja wa People's Club (MB) wakati wa uwasilishaji wa utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2005/ 2010 na 2010/ 2015 kwenye Mkutano Mkuu wa jimbo. Katika utekelezaji huo ametumia shilingi bilioni tano.
Miradi hiyo ni pamoja na kusaidia kuongeza shule za sekondari kutoka mbili hadi 15, kuwapo kwa vituo vya afya na kupeleka shule watoton15,000 wanaoishi katika mazingira magumu.
Alisema ametekeleza majukumu yake ya kusukuma maendeleo katika jimbo lake la uchaguzi kwa ushirikiano mkubwa na kufanikisha vipaumbele vya wakati huo ikiwamo elimu na afya.
Alisema kwamba kujiondoa kwake katika siasa za jimboni kunatokana na majukumu ya biashara zake kuwa makubwa pamoja na kutaka kuwa karibu na familia yake baada ya miaka 10 ya kuwatumikia wananchi wa Singida.
"Ukichukulia kuongezeka kwa-mvi kichwani, ukilinganisha wakati wa awamu ya kwanza, nafikiri ni busara sasa kutimiza majukumu haya ya familia ambayo niliyabania nafasi yake kwa kipindi cha miaka 10.
"Pia siyo siri kwamba majukumu ya biashara zangu yamebadilika katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni. Ukuaji wa biashara zangu umeambatana na kuongezeka kwa majukumu, hususan mahitaji ya muda zaidi.
Mtazamo huu wa kuipa biashara muda zaidi ni muhimu sana kwa sababu mafanikio yangu kwenye biashara ndiyo yaliyoniwezesha kuwatumikia, na yatakayo-niwezesha kuendelea kuwatumikia wananchi wa Singida kwa vitendo." alisema.
Akizungumzia sekta ya afya alisema wananchi wa Singida walifanikiwa kukabiliana vilivyo na ugonjwa hatari wa Malaria kwa kugawa vyandarua zaidi ya vyandarua 6000 kwa mama wajawazito na watoto chini ya miaka 5.
"Kwa kusambaza vyandarua hivi, tulifanyikiwa kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka 5 kwa asilimia hamsini" alisema akishangiliwa.
Aidha alishirikiana na mamlaka husika kupambana na ugonjwa sugu wa mtoto wa jicho kwa kupeleka madaktari bingwa na kufanya kambi kwenye hospital ya mkoa, waliotoa huduma ya upasuaji wa jicho na kutoa miwani kwa zaidi ya wananchi 1,000.
"Tulifanikiwa kujenga wodi ya macho, ndani ya hospitali yetu ya mkoa. Tulifanikiwa kuchangia ujenzi, wa zahanati za Mungumaji, na Manga ambazo zimekamilika! na zahanati ya kijiji cha Ititi ambao bado ujenzi unaendelea." alisema
Pamoja na ujenzi huo pia alielezea mafanikio ya kusaidia baiskeli kwa walemavu na kufunga solar panel, pamoja na majokofu ya kutunzia dawa, kwenye zahanati za Manga na Unyambwa!
Akifafanua zaidi katika sekta ya elimu alisema kwamba walijenga vyumba vya madarasa, kuweka matangi ya maji ya kuvunia maji ya mvua, vyoo, na kusambaza madawati katika shule mbali mbali za msingi na sekondari jimboni Singida mjini.
Aidha alichangia vitabu zaidi 1000, vya masomo ya sayansi na sanaa, kwa shule zetu zote, za serikali ndani ya manispaa, ya Singida na tulifanikiwa, kuwapeleka wanafunzi wa shule ya msingi Ukombozi kwenye ziara ya kujifunza bungeni.
Akizungumzia sekta ya maji walifanikiwa kuchimba visima viwili kwenye mtandao wa Suwasa na vingine 45 ndani ya baadhi ya vitongoji vyetu vya manispaa ya Singida.
Aidha alisema alifanikiwa kusukuma mradi wa visima 10, unaofadhiliwa na benki ya dunia, akisisitiza kuwa wakati akiingia mwaka 2005 upatikanaji wa maji safi na salama ulikua asilimia 23 na sasa upatikanaji wa maji umefikia asilimia 81.
Pia alisema amefanikiwa kuisukuma serikali, kujenga barabara za kiwango, cha changarawe ndani ya manispaa na kufanya manispaa kuwe na barabara zinazopitika kwa kipindi chote!
Akiwashukuru wananchi wa Singida alisema kwamba: "kuwatumikia ninyi imekuwa ni tunu kubwa sana niliyobarikiwa katika kipindi hiki cha miaka 10, na najisikia kuwa nimependelewa kwa kujifunza mambo mengi yanayohusu Singida na uongozi bora, na hususan mapungufu yake, ikiwemo mimi mwenyewe."
Alisema dhamira yake kwa wananchi haitokani na nafasi yangu kama mbunge ama mwanasiasa, akisisitiza kuwa dhamira yake ya uzaliwa inayotokana na mapenzi aliyonayo kwao na imani aliyonayo juu ya uwezo wa kuijenga Singida.
"Mapenzi yangu na imani yangu kwenu hayapimiki, na ninapenda kuwahakikishia leo kuwa, haya yatajitokeza katika njia nyingine nyingi tu."
Alisema pamoja na kutokugombea katika muhula wa tatu, lengo lake kuu la kutumikia wananchi wa Singida linabaki pale pale.
"Naomba nitoe ahadi kwenu! nitaendelea kushirikiana, na kada wa CCM, mtakaomchagua, kwenye nafasi hii ya ubunge katika shughuli zote za maendeleo ya jimbo letu! kwani dhamira yangu, ya kushirikiana nanyi, kujiletea maendeleo, haikuwa lazima mimi niwe mbunge, bali ilitokana na mapenzi yangu, kwa Singida na watu wake! "
(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog).
MSAFARA WA MR MOHAMED MSAFARA WA MR MOHAMED Reviewed by mchapishaji on 8:59 AM Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.